Kiazeri-Kusini

Kiazeri-Kusini ni lugha ya Kiturki nchini Azerbaijan, Uajemi, Uturuki, Iraq na Syria inayozungumzwa na Waazeri. Ni lugha tofauti na Kiazeri-Kaskazini ambayo ni lugha rasmi nchini Azerbaijan.

Mwaka wa 2010 idadi ya wasemaji wa Kiazeri-Kusini nchini Uajemi imehesabiwa kuwa watu zaidi ya milioni kumi na mbili. Pia kuna wasemaji milioni mbili nchini Iraq (2014), 248,000 nchini Azerbaijan, 540,000 nchini Uturuki (2014) na 44,000 nchini Syria (2014).

Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiazeri-Kusini iko katika kundi la Kiturki ya Kusini.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search